![]() |
Branislav Ivanovic akifunga bo la ushindi dakika ya 73 ya mchezo huo. |
![]() |
Jose Mourinho akizinguana na kocha mpinzani wake, Paul Lambert na Ugomvi
huo ulitokana na rafu ya Ivanovic kwa
Christian Benteke huku Refa wa akiba akijaribu kuwasuluhisha.
|
![]() |
-Christia
Benteke akishangilia bao lake alilofunga
dakika ya 45.
|
Branislav
Ivanovic Jana(Agosti 21,2013) Usiku alifunga Bao la Pili la kichwa na la
ushindi na kuipa Chelsea ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Aston Villa katika
Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Stamford Bridge lakini Meneja wa Aston Villa,
Paul Lambert, amelalamika kuhusu uamuzi wa matukio mawili muhimu kwenye Mechi
hiyo.
Chelsea
walipata Bao la kwanza baada ya shuti la Eden Hazard kuokolewa na Kipa Guzan na
kumgonga Beki Antonio Luna na kutinga wavuni dakika ya 6 ya mchezo huo.
Christian
Benteke alisawazisha kwa Aston Villa dakika ya 45 lakini Ivanovic ndio aliwapa
ushindi Chelsea dakika ya 73 ya mtanange huo.
Matukio
ambayo Aston Villa wamelalamika ni yale ya Dakika ya 69 wakati Branislav
Ivanovic alipopewa Kadi ya Njano kwa kumpiga kipepsi Christian Benteke badala
ya Kadi Nyekundu na tukio la Dakika za nyongeza wakati John Terry alipounawa
Mpira wa Kichwa cha Gabriel Agbonlahor.
Hii ni Mechi
ya Pili kwa Chelsea kushinda baada ya kuifunga Hull City Bao 2-0 katika Mechi
yao ya kwanza ya Ligi Jumapili iliyopita.
RATIBA
IJAYO YA LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi
24 Agosti,2013.
14:45 Fulham
v Arsenal
17:00
Everton v West Bromwich Albion
17:00 Hull
City v Norwich City
17:00
Newcastle United vWest Ham United
17:00
Southampton v Sunderland
17:00 Stoke
City v Crystal Palace
19:30 Aston
Villa v Liverpool
Jumapili
25 Agosti,2013.
18:00
Cardiff City v Manchester City
18:00
Tottenham Hotspur v Swansea City
Jumatatu
26 Agosti,2013.
22:00
Manchester United v Chelsea
![]() |
David Villa akishangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani FC Barcelona , aliifungia dakika ya 12 Atletico Madrid. |
Katika
uwanja wa ESTADIO VICENTE CALDERON Jana(Agosti 21,2013) Usiku ilishuhudia
Wachezaji wapya kwa Timu zao wakifunga Bao katika Mechi ya kwanza ya kugombea
Supercopa De Espana ambapo Atletico Madrid na Barcelona zilitoka sare Bao 1-1.
Timu hizi
zitarudiana huko Nou Camp Jumatano ijayo.
Bao la
Atletico Madrid lilifungwa katika Dakika ya 12 na David Villa Mchezaji ambae
alihamia Atletico akitokea Barca Mwezi uliopita.
Barcelona
walisawazisha kwa Bao la Neymar alieingizwa katika Dakika ya 59 na kufunga Bao
hilo katika Dakika ya 66 na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Barca katika Mashindano
rasmi.
Katika Mechi
hii Barca walilazimka kumpumzisha Lionel Messi wakati wa Mapumziko kutokana na
maumivu na nafasi yake kuchukuliwa na Cesc Fabregas.
![]() |
Neymar
akishangilia kuifungia klabu yake mpya, Barcelona aliyojiunga nayo kutoka kwa
dau la Pauni Milioni 48.
|
![]() |
Lionel Messi alitolewa nje baada ya kuumia katika mchezo huo wa Super Cup jana na Messi alikosa mechi kadhaa mwishoni mwa msimu uliopita kwa maumivu ya nyama mguu wa kulia. |
![]() |
(Kutoka kushoto) Carl Jenkinson, Kieran Gibbs, Theo Walcott, Aaron Ramsey
na Olivier Giroud wakishangilia bao la kwanza la -Kieran Gibbs aliloifungia
Arsenal Dakika ya 51.
|
![]() |
Olivier
Giroud akiifungia Arsenal bao la tatu kwa penalti baada ya Theo Walcott
kuchezewa rafu na Michal Kadlec kwenye boksi.
|
![]() |
Aaron Ramsey akiifungia Arsenal bao la pili katika Dakika ya 64 ya mchezo huo muhimu sana . |
Wakicheza
Ugenini huko Sukru Saracoglu Stadium Mjini, İstanbul, Nchini Uturuki dhidi ya
Fenerbahce katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONSZ LEAGUE,
Arsenal wameibuka na ushindi mnono wa Bao 3-0.
Arsenal
waliingia kwenye Mechi hii wakitoka kwenye kipigo cha Bao 3-1 katika Mechi yao
ya kwanza ya Ligi Kuu England walipochapwa na Aston Villa tena kwao Uwanja wa
Emirates Jumamosi iliyopita.
Lakini Bao 3
za Kipindi cha Pili zimewafanya wawe katika hali nzuri kwa ajili ya Mechi ya
Marudiano itakayochezwa Emirates Jumanne ijayo.
Pamoja na
Mechi ya Arsenal, pia hiyo Jana kulikuwa na Mechi nyingine 4 za kwanza za
Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Washindi wa
Raundi hii wanaingia hatua ya Makundi.
MATOKEO:-UEFA
CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA
MCHUJO-RATIBA:-Jumanne
Agosti 20,2013.
Shakhter
Karagandy 2 Celtic 0
Lyon 0 Real
Sociedad 2
Pacos de
Ferreira 1 Zenit St Petersburg 4
Viktoria
Plzen 3 NK Maribor 1
PSV
Eindhoven 1 AC Milan 1
Marudiano
Agosi 27 na 28,2013.
jumatano
Agosti 21,2013.
Fenerbahce
0 Arsenal 3
Schalke 1
PAOK Salonika 1
Steaua
Bucharest 1 Legia Warsaw 1
Ludogorets
Razgrad 2 FC Basel 4
Dinamo
Zagreb 0 Austria Wien 2
***FAHAMU:
Washindi 10 wa hii Raundi ya Mchujo wataingia Hatua ya Makundi ambapo
watajumuika na Timu 22 zinazoingia moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment