Bao pekee la
Gaudence Exavery Mwaikimba jioni ya leo, limeipa ushindi wa 1-0 Azam FC ya Dar
es Salaam katika mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Mamelodi Sundwons kwenye
Uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, uliopo Chloorkop, Johannesrbug Africa ya
Kusini.
Huo ulikuwa
mchezo wa pili kwa Azam FC katika ziara yao ya nchini hapa kujiandaa na msimu
baada ya juzi kufungwa mabao 3-0 na Kaizer Chiefs.
Katika mchezo wa leo(Agosti 07,2013), hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na wenyeji ndiyo waliotawala zaidi mchezo kipindi hicho, ingawa Azam FC walifanikiwa kutengeneza nafasi nzuri zaidi ya kufunga.
Azam FC
ilisafiri Jumamosi (03,2013) ya wiki iliyopita kuelekea afrika ya kusini kwa
maandalizi ya ligi kuu na itacheza michezo minne kama ifuatavyo.
Tarehe 5
August, Azam Fc vs Kaizer Chiefs,
Tarehe 7
August Azam Fc vs Mamelodi Sundows,
Tarehe 9
August Azam Fc vs Orlando Pirates,
Tarehe 12
August Azam Fc vs Moroka Swalows.
No comments:
Post a Comment