Wakati CECAFA limeichukua nchi ya Malawi badala ya Cameroun na Zimbabwe kama Timu ya Wageni waalikwa katika michuano ya CECAFA Tusker CHALENJI CUP 2012/2013 , Droo yapangwa huku Tanzania Bara ikitupwa kundi B. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 12, 2012

Wakati CECAFA limeichukua nchi ya Malawi badala ya Cameroun na Zimbabwe kama Timu ya Wageni waalikwa katika michuano ya CECAFA Tusker CHALENJI CUP 2012/2013 , Droo yapangwa huku Tanzania Bara ikitupwa kundi B.

Shirikisho la Soka ukanda wa Africa Mashariki na Kati CECAFA  limeichukua nchi ya  Malawi  badala ya Cameroun na Zimbabwe  kama Timu ya Wageni waalikwa kuibadili  nchini ya Djibouti katika michuano ya CECAFA Tusker CHALENJI CUP  2012/2013 ,mashindano yatakayoanza huko Nchini Uganda Novemba 24 na kumalizika Desemba 8 ,mwaka huu.




Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, amesema wameiteua Malawi kwa sababu katika Mashindano mawili ya CHALENJI CUP yaliyopita Nchi hii imeonyesha Soka safi na nidhamu ya hali ya juu.


Aidha Droo ya kupanga Ratiba za Mashindano hayo imefanyika Mjini Kampala, nchini  Uganda leo Novemba 12,mwaka huu.


Kundi A

 
Uganda 

Kenya 

Ethiopia 

Sudani Kusini  




Kundi B

Sudan Kaskazini 

Tanzania Bara 

Burundi 

Somalia


Kundi C 
 

Rwanda 

Zanzibar

Eritrea 

Malawi

Tayari Timu ya Somalia imeshawasili Nchini Uganda tangu Ijumaa iliyopita.
Wadhamini wa Mashindano haya ni East African Breweries ambao wametoa Dola 450,000 kuendesha michuano hiyo huku Mshindi akipata $30,000, Mshindi wa Pili $20,000 na wa Mshindi wa Tatu ni $10,000.


Wakati huo huo, Wenyeji wa CHALENJI CUP, Uganda, wametangaza Kikosi chao kwa ajili ya michuano hiyo na miongoni mwao ni Mastraika hatari wa Ligi Kuu Vodacom, VPL, Emmanuel Okwi wa Simba na Hamisi Kiiza wa Yanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad