Klabu ya FC
Barcelona hawajapoteza mchezo hata mmoja katika Ligi Kuu Hispania
msimu huu wakiwa wamecheza jumla ya game 31 na wameshinda game 24 na kutoka
sare game 7 pekee, kitu ambacho kinaleta dalili nzuri na muelekeo mzuri katika
mbio za kutwaa taji lao la 25 la Ligi Kuu Hispania LaLiga msimu wa
2017/2018.
Ushindi huo
umeifanya FC Barcelona kuongoza Ligi kwa tofauti ya point 11 dhidi ya Atletico
Madrid anayewafatia nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 68 na Real
Madrid akiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na jumla ya point 64.
|
Bila kujali
matokeo ya timu nyingine FC Barcelona anahitaji point 14 ili atangaze
Ubingwa wa LaLiga mapema msimu huu sawa na kupata ushindi katika game 5
wakati huu akiwa kasalia na game 7 za LaLiga mkononi, kufuatia dalili
hizo inaelezwa kuwa kuna uwezekano Barcelona akacheza El Clasico
dhidi ya Real Madrid akiwa tayari katangaza Ubingwa wa LaLiga.
Waandishi wa
habari wa Marca wameongea na kocha wa Real Madrid Zinedine
Zidane na kumuuliza ikitokea FC Barcelona akatangaza Ubingwa mchezo
mmoja kabla ya kukutana nao, ataruhusu wachezaji wake waiweke Barcelona ‘Guard
Of Honour’?
|
Hii ndio
‘Guard of Honour’ ambapo FC Barcelona waliwahi kuifanyia hivyo Real Madrid
baada ya kutangaza Ubingwa miaka kadhaa iliyopita.
“Sijui kwa nini unaniuliza swali kama hilo
lakini kiukweli mimi msimamo wangu huko wazi kabisa siwezi kuruhusu wachezaji
wangu waiwekee Barcelona ‘Guard of Honour’ kwani Barcelona ndio walivunja huo
utamaduni, hata hivyo bado mbali sana hadi Ligi kumalizika”>>>Zidane.
Zidane amefikia maamuzi hayo ya kutoruhusu
wachezaji wake waiwekee Barcelona Guard of honour ikitokea imetwaa
Ubingwa wa LaLiga kutokana na kitendo cha Barcelona kukataa
kuiwekea Real Madrid ‘Guard Of Honour’ wakati walipotoka kutwaa club
Bingwa dunia.
Kama
hufahamu Guard of Honour sio sheria bali huwa ni kitendo cha
kiuungwana (fair play) kwa wachezaji wa timu pinzani kusimama pembezoni na
kumpigia makofi timu ambayo imetoka kutangaza Ubingwa mchezo mmoja kabla ya
kukutana nao, hivyo wanaipigia makofi ikiwa inaingia uwanjani kabla ya kuanza
mchezo.
|
No comments:
Post a Comment