Watu nane
wamefariki dunia papo hapo na mmoja amejeruhiwa baada ya gari dogo aina ya
Toyota Noah waliyokuwa wakisafiria kutoka Chunya kwenda Jijini Mbeya, kugongana
uso kwa uso na basi la kampuni ya Igembesabo katika eneo la Igodima Mbeya.
|
Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Aprili 9, 2018 mchana ikihusisha Noah yenye namba za usajili T 649 DEA na basi la Igembesabo katika Barabara ya Chunya Mbeya huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa hakijulikani. |
Kwa mujibu
wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mussa Tahib ni kwamba ajali
hiyo imetokea saa 5:00 asubuhi nakusema kuwa wanafamilia hao waliofariki
walikuwa wanawahi mazishi ya ndugu yao jijini Mbeya.
|
No comments:
Post a Comment