Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera, Bw.Aidan
Bahama (kulia) akimuamulu kumwaga Pombe yake mmoja wa mwananchi aliyekutwa
akinywa pombe katika kijiji cha Ngundusi kata ya Kabanga wilayani humo April
5,2018 huku sheria ikiwataka kunywa na Wafanyabiashara ya Pombe kufanya
biashara yao baada ya saa za kazi.
Unywaji wa
pombe za kienyeji ambao wakati mwingine huambatana na baadhi ya wanywaji
kufanya vurugu, ukatili wa kijinsia, uporaji na hata kujeruhi.
|
Maafisa Watendaji
wa Vijiji na Kata wakiweno Wenyeviti wa Vijiji wilayani Ngara mkoani Kagera
wameagizwa kukomesha uuzaji na utumiaji wa pombe saa za kazi vinginevyo
watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw.Aidan
Bahama ametoa agizo hilo April 5, 2018 akiwa katika kijiji cha Ngundusi
kata ya Kabanga wilayani humo baada ya kuwakuta wananchi wamelewa saa za kazi.
Bw.Bahama amesema baadhi ya watumiaji wa pombe
katika vijiji na mitaa ni viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia sheria lakini
hawatimizi wajibu wao na kusababisha kuwama miradi ya maendeleo na watu kuwa
maskini.
"Kupitia
kwa wananchi hawa niliowakuta wanalewa asubuhi hii naagiza vijii vyote
atakayekutwa akiywa pombe saa za kazi akamatwe maana hao ndio wanachagia kuwepo
kwa umaskini" Amesema Bw.Bahama.
Maagizo hayo
ameyatoa baada ya kitembelea kijiji cha Ngundusi kata ya Kabanga akielekea
kitongoji cha Mukitamo kusalimia Familia ya Mtoto Anthony aliyemzuia Baba yake asiuze shamba licha ya familia kuwa
maskini kwa kukosa chakula na mahitaji mengine.
Hata hivyo
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kabanga wilayani Ngara Veronica Marthony amesema suala la ulevi saa za kati ni tatizo
katika vijiji akiahidi kutekeleza maagizo ya Mkurugenzi kwa kuwachukulia hatua
watakaohusiaka.
Picha/Habari Shaban Ndyamukama.
|
No comments:
Post a Comment