Mifuko ya Damu-Picha na Maktaba.
Jumla
ya Unit 204 za damu zimepatikana kutoka kwa Wananchi wakati wa zoezi la
uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu kwa hiari April
7,2018 kwenye Viwanja vya Kokoto katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Mratibu wa Damu
Salama wilayani Ngara, Mugisha
Lubagola ametoa taarifa hizo leo Aprili 9,2018 Kupitia Kipindi cha
Asubuhi Njema cha Radio Kwizera baada ya zoezi hilo kufanyika katika viwanja vya
kokoto ambapo uhamasishaji wa kuchangia damu umefanywa na Radio Kwizera ya mjini
Ngara kupitia Kampeni hiyo iliyopewa Jina la DAMU YAKO,MAISHA YANGU na itadumu
kwa miezi 6 na itafanyika mkoa wa Kigoma na Kagera kwenye wilaya zote.
|
Mwananchi wa mjini Ngara mkoani
Kagera akishiriki kuchangia Damu wakati
wa zoezi la uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu April
7,2018.
Wilaya ya Ngara huhitaji Unit 290 kila
mwezi lakini zinazopatikana kwa watu kuchangia damu ni kati ya lita 70
mpaka 85.
Kwa mujibu wa Lubagola amebainisha kuwa Binadamu
ili amchangie mwenzake damu lazima awe na umri wa miaka 18 mpaka 65 na achangie
kila baada ya miezi mitatu, awe na afya bila kuwa na magonjwa kama
kisukari ambapo siku ya kutoa damu asiwe na ugonjwa wa shinikizo la damu
(presha).
|
No comments:
Post a Comment