Emmanuel Okwi alipoifungia Simba bao
pekee la ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa huku mvua kubwa
ikinyesha, katika dimba la Jamhuri, Morogoro.
Mshambuliaji
wa Simba SC, Emmanuel Okwi ameifungia
timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom
Tanzania Bara 2017/2018 ukipigwa katika dimba la Jamhuri, Morogoro April 9,
2018.
Simba SC imeendeleza
rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi tangu kuanza kwa ligi Agosti
26, 2017.
Ni ushindi ambao unaifanya Simba SC ifikishe pointi 52 katika
mechi ya 22 ikiendeleza kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mabingwa
watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21, wakati Mtibwa Sugar
inabaki katika nafasi ya sita na pointi zake 30 za mechi 22 pia.
Mechi inayofuatia kwa Simba SC itakuwa dhidi ya Wajelajela Mbeya City FC, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. |
Tuesday, April 10, 2018
Simba SC yaongeza Pointi Muhimu za Ubingwa VPL 2017/2018.
Tags
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment