Jumla ya
Maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa
nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu.
Kauli hiyo
imetolewa Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa
akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za
Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini
Arusha.
IGP Sirro
alisema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo
kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza.
Alifafanua
kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo
walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015,
198 walifukuzwa kazi.
Alisema kwa
mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi
mwaka huu wamefukuzwa askari 14.
“Hatuna
muhali kuwachukulia hatua askari wanaokiuka utaratibu na nidhamu ya utendaji
katika Jeshi la Polisi,” alisema IGP Sirro.
|
No comments:
Post a Comment