Na:
Sylvester Raphael.
Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa ya awali na Darasa la kwanza kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2018 kipindi cha miezi mitatu na ni kipindi ambacho wanafunzi hupokelewa na kuandikishwa shuleni aidha, ifikapo Machi 31 uandikishwaji hukoma rasmi.
Mkoa wa
Kagera kwa mwaka 2018 uliotea kuandikisha wanafunzi wa awali 85,553 wavulana
wakiwa 42,678 na wasichana 42,875 lakini mkoa umefanikiwa kuvuka lengo kwa
kuandikisha wanafunzi wa Elimu ya Awali 88,343 wavulana wakiwa 44,66o na
wasichana 43,683 sawa na asilimia (103.3%).
|
Aidha katika
hatua nyingine Mkoa wa Kagera umefanikiwa kuandikisha wanafunzi wa kidato cha
kwanza kwa asilimia 90.66 na tayari wanafunzi hao wameripoti shuleni na kuanza
masomo yao ya sekondari.Wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na Elimu
ya Sekondari wavulana walikuwa 17,191 na wasicha 17,971 jumla 35,161.
Wanafunzi
walioripoti katika shule za Sekondari Mkoani Kagera hadi kufikia Machi 31, 2018
jumla ni 31,877 sawa na asilimia 90.66 wavulana wakiwa 14,814 sawa na asilimia
86.173 na wasichana 17,063 sawa na asilimia 94.953.
Mkoa
unaendelea na juhudi za kuwafuatilia wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni
kuhakikisha wanaripoti mara moja ili kuendelea na masomo ya kidato cha
kwanza.
Aidha,
uongozi wa Mkoa wa Kagera unatoa rai kwa wazazi na walezi wa wanafunzi ambao
bado hawajaripoti shuleni kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti vinginevyo
wazazi na walezi watauchukuliwa hatua za kisheria kwa kutowapeleka watoto wao
shule.
Vilevile
Mkoa wa Kagera unaendelea na juhudi za kuweka mazingira mazuri ya kujifunza na
kujifunzia ili kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
Pia kuhakikisha mkoa unashika
nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na ufaulu wa maksi za juu kama ilivyo
desturi ya Mkoa wa Kagera.
|
No comments:
Post a Comment