Mkuu wa
Wilaya ya Chato,mkoani Geita, Bw. Shaaban Ntarambe amesema wataalamu wa kilimo vijijini wanao
wajibu mkubwa katika kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya chakula na Biashara
unaongezeka na kukidhi mahitaji ya jamii na masoko.
Mkuu wa
Wilaya ameyasema hayo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kilimo wilayani
hapa ziara ambayo ameifanya kwenye tarafa zote tano ambapo ziara hiyo pia
ilikuwa na lengo la kujitambulisha kwake tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Wilaya
hiyo mwezi Oktoba, 2015 .
Akiongozana
na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mkuu wa Wilaya amewaagiza wataalamu
wote wa kilimo kutokukaa ofisini na badala yake watembelee wakulima na
kuwashauri juu ya kilimo bora na kanuni zake, “Najua wengi wenu mpo likizo,
mubadilike kwani vigezo vya kupendana katika kazi viwe katika misingi ya kazi
wasaidieni wakulima” alisema Mkuu wa Wilaya.
Mbali na
kusitiza juu ya kilimo cha Pamba Mkuu wa Wilaya pia amewaagiza wataalamu hao
kuhakikisha wanakuwa na mashamba ya mfano katika maeneo wanayosimamia ili iwe
rahisi hata kwa wakulima kujifunza kupitia mashamba hayo. Mashamba ya mfano
yaliyosisitizwa ni ya mazao yote ya msingi yanayolimwa wilayani hapa ambayo ni
Mpunga, Alizeti, Mahindi na Mhogo.
Bw. Ntarambe
amewaagiza maafisa ugani wote kuhakikisha wanapima mashamba ya wakulima wote
waliopo wilayani Chato ili kuwa na takwimu sahihi za eneo lililolimwa msimu wa
2015/2016.
|
No comments:
Post a Comment