Akitoa neno
kwa wananchi hao
ambao ni wahanga
wa maafa hayo
kabla ya kushiriki
zoezi la kuwagawia
mahindi wananchi mkuu
wa Mkoa wa
Kagera amesema kuwa
serikali itaendelea kuwajali
wananchi wake kwa
wakati wowote ule
pindi majanga yanapojitokeza kwani
siku zote serikali
ipo kwa ajili
ya kuwasaidia wananchi
wake.
|
Amesema zoezi
hilo la kutoa
msaaada wa chakula
kwa wahanga hao
lisihusishwe na kampeini
za vyama vya
siasa zinazoendelea kwa sababu
hakuna anayeomba maafa
yatokee ili anayeomba
kura aitumie kama
fursa ya kujipatia
umaarufu au kura.
|
Mkuu wa
wilaya ya Karagwe
Deodatus Kinawiro awali akisoma taarifa
ya wilaya amesema
kuwa kata zilizoathiriwa na mvua
hizo zilizonyesha Agosti 31 na
Septemba 3 mwaka huu,2015 kuwa ni kata za Kihanga, Kanoni, Igurwa na
sehemu ndogo ya
Kata ya Bugene
amesema wilaya ya
Karagwe walikuwa wameomba
kupatiwa tani 48
za mahindi lakini
wamepatiwa tani 40
na tani 16
za maharage walizokuwa
wameomba hazikuweza kupatikana.
|
No comments:
Post a Comment