Baba Askofu Severin Niwemugizi na Dr Sengati kulia.
Wanachama
watatu wa Chama cha Mapinduzi wilayani Ngara Mkoani Kagera wamechukua Fomu za Kuwania
Ubunge wa Jimbo la Ngara ikiwa ni siku moja tangu kuanza kwa zoezi la kutoa
Fomu za Ubunge na Udiwani.
Katibu wa
Chama cha Mapinduzi wilayani Ngara Bw Jacob Makune amewataja waliochukua Fomu
hizo kuwa ni Bw Cyprian Muheranyi, Bi Hellena Adrian Ghozi na Dr Philemon Sengati.
Akizungumza
na Radio Kwizera Bw Cypriuan Muheranyi ambaye ni Mgombea wa kwanza kurudisha
Fomu hiyo baada ya kuichukua hapo jana Julai 15,2015, ametoa wito kwa wakazi wa
Ngara kujiepusha na vitendo vya Rushwa wakati wa Uchaguzi ili kupata viongozi
bora watakaochochea Maendeleo.
Katibu wa
CCM wilayani Ngara amesema zoezi la utoaji wa Fomu za Ubunge linakwenda pamoja
na utoaji wa Fomu za Udiwani kwenye Ofisi za CCM katika Kata za wilaya hiyo
,likianza jana Julai 15 hadi Julai 19,2015 ambapo ametoa wito kwa Wanachama wenye sifa kujitokeza kuchukua Fomu hizo.
Source:-Radio
Kwizera.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment