MGOGORO BURUNDI:-Taswira Picha Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, alivyokutana na wadau ili kujaribu kuutafutia suluhu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 16, 2015

MGOGORO BURUNDI:-Taswira Picha Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, alivyokutana na wadau ili kujaribu kuutafutia suluhu.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mjini Bujumbura, Julai 14 mwaka 2015.

Baada ya kukutana Jumanne jioni wiki hii na upinzani na vyama vya kiraia, Yoweri Museveni anatazamiwa  mapema Jumatano asubuhi kakutana na wajumbe wa serikali, na baadae marais wa zamani. Yoweri Kaguta Museveni atahitimisha kazi yake hiyo kwa mkutano wa pamoja na wadau wote katika mzozo wa Burundi.

Rais Yoweri Kaguta Museveni aliwasili mjini Bujumbura Jumanne mchana Julai 14,2015, Rais Yoweri Kaguta Museveni aliingia nchini Burundi kwa gari akipitia mkoani Kirundi Kaskazini mwa Burundi, kwenye mpaka na nchi ya Rwanda.

Rais Museveni alishiriki mara kadhaa katika mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi hadi kupatikana kwa Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha. Wakati huo rais Museveni alikua rais wa jitihada za kikanda kwa ajili ya mazungumzo ya Mkataba huo.

Hata hivyo Upinzani umesema hauna matumaini kwa vikao hivyo kuwa vitazaa matunda yoyote, kwani, hasa kuwa rais Museveni hana uwezo wa kutafutia suluhu mzozo wa Burundi, ambapo chanzo cha mzozo huo ni muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza, wakati msuluhishi huyo mpya mwenyewe ana nia ya kuwania muhula mwengine katika uchaguzi wa urais, huku wapinzani nchini mwake wakiendelea kukandamizwa.


Rais Museveni aliteuliwa Julai 6,2015 kama mpatanishi mpya katika mkutano wa kilele wa mwisho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Dar es Salaam, nchini Tanzania.

Upinzani ulilani na kutupilia mbali maazimio ya mkutano huo, ukitaja kwamba unamtetea rais Nkurunziza, lakini kambi ya rais ulikaribisha maazimio hayo.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad