UBUNGE NGARA:-Dr.Bujari arudisha fomu CHADEMA na kuahidi kukuza uchumi wa Wanangara na kuwa wa kati akipewa Dhamana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 18, 2015

UBUNGE NGARA:-Dr.Bujari arudisha fomu CHADEMA na kuahidi kukuza uchumi wa Wanangara na kuwa wa kati akipewa Dhamana.

Pichani ni   Muomba ridhaa ya  Ubunge Jimbo la Ngara kupitia  Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiongea na Wana  Ngara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana June 17, 2015 kwenye uwanja wa Posta ya zamani ambapo pamoja na mambo Mengine  amerudisha fomu ya kuomba kuteuliwa na CHADEMA na kusema iwapo Chama chake kitampitisha na kuchaguliwa na Wana Ngara, atahakikisha anashirikiana nao kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kuwa na uchumi wa kati sambamba   na kukuza Uchumi wa Ngara,kuongeza ajira kwa vijana kupitia fursa zilizopo,kusimamia sheria ili kutatua migogoro ya ardha na kuhimiza na kutetea mafao ya wastaafu.



Katika mkutano huo wa jana June 17, 2015, Baadhi ya Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema mjini Ngara Mkoani Kagera wamechanga zaidi ya Sh Elfu 70 na kisha kumchukulia Fomu ya kuwania Udiwani Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani Ngara Bw Kenedy Staford.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya Mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika kwenye Viwanja vya Posta ya zamani mjini Ngara ambapo baadhi ya wafuasi wa Chama hicho wameonekana wakiwa wamebeba mabango yanayomshawishi kiongozi wao huyo atangaze nia na kuchukua Fomu ya kugombea udiwani Kata ya Ngara Mjini.

Wafuasi hao wa Chadema wamesema wamefikia uamuzi wa kuchanga fedha hizo ili kumuwezesha kiongozi wao kuwania Udiwani Ngara Mjini bila kutumia gharama za kuchukua Fomu ambazo ni Sh elfu 50.

Aidha Bw Kenedy amesema ameridhia matakwa ya wananchi hao na kwamba atajaza Fomu hiyo kuomba Ridhaa ya Chama chake ili kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad