Katibu wa
NEC; Itikadi na Uenezi CCM taifa Nape Nnauye.
Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kimelaani vikali vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Chadema na
CUF kwa viongozi wa serikali za mitaa katika maeneo kadhaa nchini ikiwemo mikoa
ya Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya.
Akizungumza
na waandishi wa habari Katibu wa NEC; Itikadi na Uenezi CCM taifa, Nape Nnauye
amesema vurugu hizo mbali na kuhatarisha na kuharibu mali pia zilizosababisha
baadhi ya viongozi wa CCM kujeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali.
Amesema
vurugu hizo zimetokea katika mkoa wa Mwanza ambapo Christopher Mgeta kutoka
Mtaa wa Ibungilo na Pascal Charles wa Mtaa wa Kitangiri A katika wilaya ya
Ilemela walivamiwa na kupigwa wakati wa kuapishwa.
Alieleza
kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, Sultan Jeta wa mtaa wa Ukwamani katika
jimbo la Kawe alifanyiwa fujo na wafuasi hao na Mtaa wa Msisiri A Kata ya
Mwananyamala katika Jimbo la Kinondoni Juma Mbena alipigwa na kuvunjwa mkono.
“Katika
Manispaa ya Ilala, wafuasi wa vyama vya upinzani walifanya vurugu wakati wa
kuapishwa kwa viongozi wa serikali za Mitaa, jambo lililopelekea zoezi hilo
kuahirishwa.
Nnauye
amesema katika Mkoani Mbeya pia vurugu za aina hiyo zimetokea katika wilaya za
Kyela na Rungwe ambapo wilayani Kyela zoezi la kuapisha viongozi wa serikali za
mitaa lilishindika na kuahirishwa kutokana na vurugu za kurushiwa mawe
zilizofanywa na wafuasi wa Chadema walioletwa kutoka katika maeneo mbalimbali
ya Mkoa huo.
Aliongeza
kuwa katika Kijiji cha Ilundo wilayani Rungwe wafuasi hao wa Chadema waliwapiga
mawe viongozi na wanachama wa CCM na baadae kufyeka mashamba yao ya migomba na
kusababisha vijana sita kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya
Rungwe kwa sababu ya hasira za kushindwa uchaguzi.
“Vurugu hizi
ni mwendelezo wa tabia na mazoea ya vyama vya upinzani nchini kutoheshimu na
kufuata sheria na taratibu za nchi, tabia hizi si za kiungwana na
ni uthibitisho wa kuharibikiwa na kufa kwa vyama vya upinzani nchini.
Mara zote
wamekuwa wakikataliwa na wananchi kwa kura, wao hukataa uamuzi huo wa wananchi
kwa kufanya fujo na vitimbi, ”amesema Nnauye.
|
No comments:
Post a Comment