TANZIA:-Picha za Matukio ya Msiba wa Mtoto wa Raila Odinga wakati Mwili wake ulipowasili Mjini Kisumu ,Kuzikwa Leo Januari 10,2015 eneo la Bondo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 10, 2015

TANZIA:-Picha za Matukio ya Msiba wa Mtoto wa Raila Odinga wakati Mwili wake ulipowasili Mjini Kisumu ,Kuzikwa Leo Januari 10,2015 eneo la Bondo.

Mwili wa Marehemu, Mtoto wa kwanza wa Waziri mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, alifariki usiku wa Jumamosi Januari 03 kuamkia Jumapili Januari 04,2015 katika mazingira ambayo hayajawekwa bayana ukishushwa kwenye ndege.....Fidel Odinga, alikuwa akirudi nyumbani usiku katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.


Januari 09,2015,Asubuhi,Mwili wa marehemu Fidel Odinga ulisafirishwa na Ndege ya Jeshi la kenya ,Kenya Air Force hadi katika mji wa Kisumu ambapo msafara wake utaanzia hapo hadi kwenye kijiji cha Bondo kwenye makazi ya Baba yake ,Bw.Raila Odinga kwa ajili ya maziko leo Jumamosi Januari 10,2015.

Fidel Odinga alikutwa amekufa nyumbani kwake katika kata ya Karen, ambako alikua akiishi na mke wake wa pili mwenye asili ya Eritrea na mtoto wao mdogo.

Fidel Odinga alikua akirudi nyumbani usiku wa manane akitokea katika burudani na marafiki zake katika hoteli Sankara katika eneo la Westlands.

Mtoto huyo wa kwanza wa Raila Odinga, alizaliwa mwaka 1973, na aliitwa jina la Fidel kwa heshima ya Fidel Castro, rais wa zamani wa Cuba, wakati baba yake na babu yake walikuwa wote walidhamiria katika itikadi za kikomunisti.

Fidel Odinga ambaye ni miongoni mwa watoto wanne wa Raila Odinga, alikua akipewa nafasi kubwa ya kumrithi kisiasa baba yake.




UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad