
Taarifa za nchini humo
zinaeleza kuwa, ukarabati huo wa jumba lake gharama zake zote zinatarajiwa
kulipwa na serikali.
Kufuatia hatua hiyo,
uchunguzi umeanza kuhusu ukarabati huo ambao ni nyumba yake binafsi Rais Jacob
Zuma.
Tangazo limetolewa na
ofisi ya Mhifadhi wa Masilahi ya Wananchi, baada ya magazeti kutuhumu kwamba
ukarabati unaopangwa kufanywa kwenye nyumba ya Rais Zuma utaogharimu dola
milioni 25, karibu wote unatarajiwa kulipwa na serikali.
Msemaji alieleza kuwa
kamati ya uchunguzi imewasiliana na ofisi ya rais kuhusu ujenzi huo kwenye
nyumba ya Rais Zuma ilioko Nkandla katika jimbo la KwaZulu-Natal.
Hata hivyo Serikali yake
imetetea uamuzi huo na kueleza kwamba ujenzi huo unafuata kanuni
rasmi.
Source:BBC Swahilli.
No comments:
Post a Comment