
Barcelona ndio wanaongoza La Liga
hadi sasa wakiwa Pointi 8 mbele ya Real Madrid ambao wako nafasi ya 6.
MSIMAMO TIMU :
1 Barcelona Mechi 6 Pointi 18
2 Atletico Madrid Mechi 6
Pointi 16
3 Malaga Mechi 6 Pointi 14
4 Real Betis Mechi 7 Pointi 12
5 Real Mallorca Mechi 6 Pointi
11
6 Real Madrid Mechi 6 Pointi
10
7 Real Valadoid Mechi 7 Pointi
10
HALI YA KILA TIMU:
FC Barcelona
Barcelona wataingia kwenye Mechi
ya leo bila ya Kepteni wao Carles Puyol na pengine bila ya Sentahafu wao
mwingine Pique ambae alikuwa akiuguza mguu wake.
Mapengo hayo huenda
yakamlazimisha Kocha wa Barca Tito Vilanova kuwachezesha Viungo Alex Song na
Mascherano kama Masentahafu huku Jord Alba na Alves wakicheza kama Mafulbeki.
Kwenye Kiungo ndiko injini ya
Barca na, bila shaka, watakuwepo Xavi, Busquets na Iniesta.
Mbele Supastaa Lionel Messi
anaweza kushirikiana na Pedro huku David Villa akitinga dimbani baadae kwenye
Mechi pamoja na Chipukizi Tello.
Kikosi kinaweza kuwa [Mfumo
4-3-3]: Valdes; Alves, Mascherano, Song, Alba; Xavi, Busquets, Cesc; Messi,
Pedro, Tello.
Real Madrid
Kwa Mameneja wangu kuwa Pointi 8
nyuma ya Timu ambayo inasifika ni bora Duniani kunaweza kuwatia mchecheto
lakini si kwa Jose Mourinho ambae hujisifia wenyewe kuwa ni ‘Mtu Spesheli’ na
sasa akijiita ‘Mtu pekee.’
Kikosi cha Real ni imara na
kimesheheni Wachezaji mahiri kuanzia Kipa Iker Casillas hadi mbele kwa Supastaa
Cristiano Ronaldo.
Upo kila uwezekano Difensi yao
ikawa na Arbeloa, upande wa kulia, Masentahafu Pepe na Ramos na Beki wa kushoto
ni Marcelo.
Kwenye Kiungo, Jose Mourinho ana
Wachezaji kibao wa kuwachagua na upo uwezekano Ricardo Izecson dos Santos
Leite, maarufu kama Kaka, akapata muda wa kuonekana Uwanjani baada ya kuonyesha
cheche zake kwa mara nyingine tena hivi karibuni.
Viungo wengine wanaoweza kuwepo
ni kati ya Alonso, Khedira, Ozil, Di Maria, Essien na Modric.
Kikosi kinaweza kuwa [Mfumo
4-2-3-1]: Casillas; Arbeloa, Ramos, Pepe, Coentrao; Alonso, Khedira; Ozil,
Di Maria, Ronaldo; Benzema.
DONDOO MUHIMU:
-WAMECHEZA MARA 221: Ushindi
Barca 87 Real 88 Sare 37
-MECHI NYINGI EL CLASICO:
Xavi, 34 kwa Barca, Raul 37 kwa Real
-BAO NYINGI: Messi, 15 kwa
Barca, Alfredo Di Stefano kwa 18
Imeandikwa na Soka in Bongo.
No comments:
Post a Comment