Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Watoto wa Kike yaanza kutolewa Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 24, 2018

Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Watoto wa Kike yaanza kutolewa Mkoani Kagera.

Nesi akitoa Chanjo  ya Saratani ya mlango wa shingo ya kikazi wakati wa uzinduzi huo Kimkoa,katika Kituo cha Afya Kaigara wilayani Muleba mkoani Kagera.

Wasichana 35,917 wenye umri wa miaka 14 mkoani Kagera wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi kwa mwaka mzima huku wakihimizwa wazazi na walezi kuwapeleka Wasichana hao kwenye  katika vituo vya kutolea huduma za Afya 1,182.
Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu  akizindua zoezi la chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi inayotolewa mkoani humo kuanzia Jana April 23,2018.

Wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo hiyo ambapo kimkoa imezinduliwa katika Kituo cha afya cha Kaigara wilayani Muleba,Mkuu wa Mkoa amewataka Wakuu wa Wilaya wote mkoani humo, kusimamia kwa ukamilifu zoezi hilo kwani linatolewa bure hivyo ni wajibu wa wazazi na walezi kuhamasisha wasichana kujitokeza kwa wingi.

Dalili za ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ni kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kuvimba miguu, kutokwa na usaha wa rangi ya kahawia katika sehemu za siri za mwanamke.


 Aidha, visababishi vya ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, na kuvuta sigara.


Ili kujikinga na ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ni muhimu sana wasichana wakazingatia kutojihusisha na visababishi vilivyotajwa hapao juu.


Pia Katika Mkoa wa Kagera kuna vituo vipatavyo 56 vinavyohusika na uchunguzi wa awali wa ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo mkoa unatoa wito kwaakina mama kuwahi mapema katika vituo hivyo pale wanapohisi dalili hizo ili kufanyiwa uchunguzi mapema.

Post Bottom Ad