Inadaiwa
kuwa mnamo Julai 10, 2010 katika Kijiji cha Yulansoni Kata na Tarafa ya
Kinyangiri Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Tabu Robert (28) ambaye kwa kabila
ni Mnyiramba, Mkulima wa Yulansoni, aliuawa na Mume wake aitwae Bernard Shumba
Siza (47), Mnyiramba na mkulima wa Yulansoni.
|
Baada ya
Mmuhumiwa kufanya tukio hilo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuficha
kwenye mti wa mbuyu ambao una tundu kubwa na kisha aliripoti Polisi kituo
kidogo cha Kinampanda Mkalama kuwa Mke wake ametoroka na alianza kumtafuta hadi
tarehe Machi 17, 2018 ambapo taarifa zilipopatikana kuwa alimuua.
|
Baada ya
mtuhumiwa kukamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kuonyesha
sehemu alipouficha mwili huo Machi 18, Mwaka huu,2018 majira ya saa 10:00 jioni.
Mkuu wa
Polisi Kituo cha Mkalama na timu yake ya
Makachero walifika eneo la tukio na kufanikiwa kupata mabaki ya mifupa yakiwa
ndani ya mti huo. Baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa
mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi.
|
No comments:
Post a Comment