Taswira Picha: Mawaziri Ndalichako,Masauni watoa mkono wa pole Wafiwa Kifo cha Mwanafunzi aliyepigwa risasi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 18, 2018

Taswira Picha: Mawaziri Ndalichako,Masauni watoa mkono wa pole Wafiwa Kifo cha Mwanafunzi aliyepigwa risasi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Injinia Hamad Masauni  wakimfariji Mama Mzazi wa marehemu  Aqwilina jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar.

Mwanafunzi  huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha CHADEMA.Kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo Serikali imesema itabeba jukumu la Mazishi yake.

Aidha Rais Dkt John Pombe Magufuli  amesema amesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi huyo,Aqwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).

"Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili",Ilisema sehemu ya taarifa yake iliyotolewa mapema leo february 18,2018.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako (tatu kulia) akiwafariji Mama Mzazi wa marehemu  Aqwilina pamoja na ndugu jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar es Salaam.
Mama wa Marehemu Akwiline akilia kwa uchungu mara baada ya kuona viongozi wa Waandamizi wa serikali walipofika nyumbani kwake,Mbezi Kimara jioni ya leo kwa lengo la kutoa pole na kufahamu taratibu mbalimbali za msiba huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad