Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT), Akwiilina Akwilina enzi za uhai wake.
Waziri Ndalichako
amesema kuwa viongozi mbalimbali wameguswa na kifo hicho kwani mwanafunzi huyo
hakuwa na hatia yoyote na kusema kifo chake ni pigo kubwa kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Marehemu Akwilina alikua ni miongoni mwa
wanaufaika wa mikopo ya elimu ya juu, wizara yangu itamkumbuka marehemu
Akwilina kama mmoja ya wanafunzi wa kike ambao wamejipambanua katika kutambua
na kuthamini umuhimu wa elimu na hivyo kuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha
anasoma kwa bidii kwa manufaa yake mwenyewe, familia yake na manufaa mapana ya
taifa letu kwa ujumla”
Ndalichako
amedai kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kimetokea wakati akiwa kwenye harakati ya
kupeleka barua ya maombi ya mafunzo kwa vitendo ambayo alikuwa akitegemewa
kuanza Februari 26, 2018 na kudai kifo hicho kimezima ndoto yake na serikali
kukipokea kwa masikitiko.
“Mimi Waziri mwenye dhamani ya elimu nimesikitika
sana kuona binti huyo amepoteza maisha akiwa katika kutekeleza shughuli zake za
kielimu, Wizara yangu itagharamia mazishi ya marehemu Akwilina hadi hapo
atakapopumzishwa katika makao yake ya milele, namuagiza Katibu wangu kuakikisha
kwa pamoja tunasimamia shughuli zote za msiba huu”
Aidha Waziri
waliviomba vyombo vya usalama kufanya uchunguzi kwa haraka ili kuwatambua na
kuwakamata watu ambao wamesababisha kifo cha mwanafunzi huyo ili hatua za
kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
|
Sunday, February 18, 2018
Mazishi ya Mwanafunzi wa NIT, Akwilina kugharamiwa na Serikali.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment