VPL 2017/2018 -Singida United yaigonga Lipuli FC,Kesho Simba SC na Tanzania Prisons Mbeya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 17, 2017

VPL 2017/2018 -Singida United yaigonga Lipuli FC,Kesho Simba SC na Tanzania Prisons Mbeya.

Singida United imepanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya tano baada ya ushindi wa leo November 17,2017 wa  bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Namfua, Singida.

Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ifikishe pointi 17 baada ya kucheza mechi 10 na kuishusha Prisons nafasi ya sita. 

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Jonesia Rukyaa wa Kagera aliyesaidiwa na Lulu Mushi wa Dar es Salaam na Geoffrey Msakila wa Geita, bao pekee la Singida lilifungwa na nyota wa Rwanda, Danny Usengimana dakika ya 82 akimalizia krosi ya Salum Chuku kutoka upande wa kushoto.

Tanzania Prisons wanaweza kurudi juu ya Singida kesho iwapo watashinda dhidi ya Simba SC kesho Jumamosi November 18,2017 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Simba SC itakuwa na kazi ya kuhakikisha inaondoka na pointi tatu ili kupata zote sita mkoani Mbeya.

Mechi nyingine za kesho Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Stand United na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Maji Maji na Mbao FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea na Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mzunguko wa 10 utakamilishwa kwa michezo miwili, Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, Yanga watakuwa wenyeji wa Mbeya City na Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, wenyeji Njombe Mji FC wataikaribisha Azam FC.

Simba inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 19, sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao, wakati Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 17, sawa na Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad