Taswira Picha za Eneo la ajali ya Ndege iliyoua Watu 11 Ngorongoro -Arusha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 16, 2017

Taswira Picha za Eneo la ajali ya Ndege iliyoua Watu 11 Ngorongoro -Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limepata miili ya watu 11 waliofariki kwenye ajali ya ndege ndogo ya Coastal Aviation iliyotokea jana November 15, 2017 katika eneo la Embakaai Wilayani Ngorongoro wakati ikiwa safarini kuelekea Serengeti.

Ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja mdogo wa Arusha saa nne na dakika 10 asubuhi kuelekea uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KIA) na Shirika la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali  hiyo limesema kuwa watu wote 11 waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki dunia.

Coastal wameeleza kuwa, ndege yao, Cessna Caravan ilipata ajali majira ya saa 5 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na Kwa sasa unafanyika uchunguzi katika eneo la tukio na kuwa, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo watazitoa mara taarifa kamili zitakapopatikana.

  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad