Rubani anapoamua Kuchora angani Sehemu Nyeti. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 18, 2017

Rubani anapoamua Kuchora angani Sehemu Nyeti.

Maafisa wa jeshi la wanamaji wamesema kwamba haikubaliki kwamba mmoja wa marubani wake alitumia ndege moja ya kijeshi kuchora uume wa mwanadamu angani.

Mchoro huo uliokuwa katika kaunti ya Okanogan magharibi wa jimbo la Washington nchini Marekani ulizua hisia nyingi katika mitandao ya kijamii.

Lakini makomando katika kituo hicho cha wanamaji kilichopo katika kisiwa cha Whidbey hawakuona ucheshi wake na sasa wameanzisha uchunguzi.

Msemaji wa kambi hiyo ya kijeshi alithibitisha kuwa ndege iliohusika kuchora uume huo kwa kutumia moshi wake ni ile ya Boeing EA-18G Growlers.

Onyo: Baadhi ya watazamani huenda wakaona picha hizi kama zisizo na maadili.  
Rubani wa ndege ya Marekani alichora Uume angani.

Ndege hiyo hutumika maalum kwa vita vya kielektroniki na inaweza kusafiri mara mbili kasi ya sauti.

Msemaji Thomas Mills aliambia BBC : Mimi kama mwanamaji tunawapatia heshima kubwa marubani wetu na hili halikubaliki hata kidogo.

Watazamaji waliokuwa chini ardhini walichekeshwa na mchoro huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad