VPL 2017/2018 -Mbao FC kuwagomea Simba SC kesho –CCM Kirumba.?? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 20, 2017

VPL 2017/2018 -Mbao FC kuwagomea Simba SC kesho –CCM Kirumba.??

Simba SC ina nafasi kubwa ya kuharibu hesabu za Mtibwa Sugar ikishinda mchezo wa kesho September 21,2017 dhidi ya Mbao FC kwa kuiondoa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2017/2018 utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Simba SC ambayo kwa sasa ina pointi 7 ikiibuka na ushindi kwenye mchezo huo itafikisha alama 10 na kuishusha kileleni Mtibwa Sugar yenye pointi 9 ikiwa imecheza mechi tatu.

Tayari Simba SC imecheza mechi tatu za Ligi Kuu msimu huu, ikishinda mechi mbili  kwa bao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na 3-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, wakati mwingine wametoka sare ta 0-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Katika mabao 10 iliyovuna kwenye mechi mbili, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi amefunga mabao sita, manne dhidi ya Ruvu na mawili dhidi ya Mwadui, sasa akiwa anaongoza kwa kufunga katika Ligi Kuu. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad