Peter Msigwa Kuripoti kwa RCO Leo September 25, 2017 baada ya Dhamana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 25, 2017

Peter Msigwa Kuripoti kwa RCO Leo September 25, 2017 baada ya Dhamana.

Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Petter Msigwa ameachiwa huru Jana,September 24,2017, usiku  kwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Msigwa aliachiwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa BAVICHA- Iringa  Leonce Marto , saa nne usiku .

Msigwa alishushwa  Jukwaani kwa nguvu  akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .

Marto  amesema  mikutano yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine  mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo.

Leo,Jumatatu September 25,2017,  Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani .

Amesema  Mbunge huyo  atazungumza na vyombo vya habari leo mchana  kuweka wazi madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad