|
Maonesho ya Kilimo (NaneNane) yanataraji kuanza leo, Agosti 01, 2017 kote
nchini kwa ngazi mbalimbali za kanda huku Maonesho hayo Kitaifa yakifanyika Mkoani
Lindi wakati Maandalizi na maonesho
ya Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi
wa mikoa husika.
Maandalizi ya Maonesho ya 24 ya Kilimo na sherehe za Nane nane
yatafanyika kwa siku 8 ambapo Kitaifa yatafika ukomo jioni ya Agosti 8, 2017
katika Viwanja vya Ngongo na Maeneo mengine yatakapoadhimishwa kikanda katika
Viwanja vya maonesho ni John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere
–Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni -
Dodoma; Nyahongolo – Mwanza; na Fatuma Mwassa - Tabora.
Maonesho ya Mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo hutoa changamoto ya
kuleta Mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa
vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.
|
|
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg
Mathew Mtigumwe wakati akizungumza na Wanahabari kueleza muktadha wa
Maonesho hayo ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi na kubebwa na kauli mbiu
mahususi kwa mwaka huu 2017 isemayo "Zalisha kwa Tija Mazao ya Bidhaa za
Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati"
Ndg.Mtigumwe amesema
kuwa Wizara, Taasisi/Makampuni ya Umma na Binafsi, Mabenki na Wadau wote wa Kilimo
na Mifugo wataendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza
uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda
vinavyokusudiwa kuanzishwa.
Malengo ya maonesho hayo ni utoaji elimu ya matumizi ya teknolojia
mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na
kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi.
|
|
Teknolojia au Bidhaa zitakazooneshwa ni pamoja na Zana za Kilimo, Mbegu bora
za Mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa
ambapo piaTaasisi za kitafiti ambazo zitaonyesha teknolojia mbalimbali za
kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa
chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na
mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi
wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa.
Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za
kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano,
ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za
asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali,
na Nta.
Maonesho ya Sikukuu ya
Wakulima Nanenane yanahusisha shughuli za Wakulima, Wafugaji wa Mifugo, Wafugaji
wa nyuki, Wavuvi, Wanamazingira, Wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na
mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi
za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali. |
|
Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote
tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja
wanaoshughulika na kilimo.
Miaka ya 1990 sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba7,July kila
mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya
kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa ambapo
lengo la serikali likawa kuitumia Saba Saba kama siku ya maonyesho ya Biashara
ya Kimataifa, ambapo Wafanyabiashara wengi walijitokeza ama hujitokeza
kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha na siyo kuwafundisha Watanzania mbinu za
kuzalisha biadhaa hizo.
Picha zaidi Hapa chini zinaonyesha maandalizi ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja
vya Ngongo Mkoani Lindi
|
|
Habari/Picha-Na Mathias Canal, Lindi
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment