Taswira Picha Uogeleaji wa utupu Finland ili kuvunja rekodi. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 18, 2017

Taswira Picha Uogeleaji wa utupu Finland ili kuvunja rekodi.

Ilikuwa ili kuvunja rekodi lazima kuogelea mara ya tatu .

Mamia ya waogeleaji waliokuwa utupu walijumuika kwa pamoja kuogelea katika mto wenye maji baridi katika jaribio la kuvunja rekodi nchini Finland.

Washiriki walikuwa wanataka kuvunja rekodi ya dunia ya watu wengi zaidi kuwahi kuogelea kwa pamoja wakiwa utupu.

Watu 789 waliokuwa pia wanahudhuria tamasha ya muziki mashariki mwa Finland walijitosa kwenye maji kuogelea wakiwa utupu, waandalizi wanasema.

Walifanikiwa kuvunja rekodi ya awali iliyokuwa imewekwa na waogeleaji nchini Australia, kwa kuzidi watu hao kwa watu watatu, taarifa zinasema.

Waandalizi wamesema sasa wanasubiri rekodi yao ithibitishwe na maafisa wa Guinness World Records.

Hii ni mara ya tatu kwa jaribio la kuvunja rekodi hiyo kuandaliwa nchini Finland, mtandao wa habari wa Yle umesema.

Rekodi waliokuwa wakijaribu kuivunja iliwekwa mwaka 2015 mjini Perth na watu 786 waliokuwa wanajaribu kuhamasisha watu kuipenda miili yao.

Kuogelea nje kwenye mito na bahari ni utamaduni wa miaka mingi nchini Finland, ambapo "avantouinti" - kuogelea katika shimo la barafu - hutangazwa na bodi ya utalii nchini humo kama shughuli inayosaidia kusisimua mwili.


Post Bottom Ad