Akiwa njiani
kuelekea Ngara, Mhe. Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa Nyakahura
ambapo amewahakikishia kuwa Serikali itaifanyia matengenezo ya barabara ya
Nyakahura – Rusumo – Ngara, ameahidi kumtuma Waziri wa Maji na Umwagiliaji
kwenda kuangalia namna ya kutatua tatizo la maji na pia amechangia Shilingi
Milioni 10 katika ujenzi wa majengo ya shule.
Kesho Alhamisi, tarehe
20 Julai, 2017 Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Kagera ambapo
hapa Ngara atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika
mchana.
|
Umati
Waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa
kilometa 154,wakimshangilia,Mh Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Joseph Magufuli, mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa
ufunguzi wa barabara kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo 19 Julai 2017.
|
Rais wa
Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akipungia
vikundi vya kwaya,ngoma na Burudani alipowasili kwenye viwanja vya stendi ya
Biharamulo tayari kwa kuzindua Barabara ya Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye
urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya
siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Barabara hiyo imejengwa
kwa gharama ya Shilingi Bilioni 190.4 zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment