Picha- Rais Magufuli Akitoa siku 14 kwa Wamiliki wa Vituo vya Mafuta Nchini kutumia (EFDs). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 19, 2017

Picha- Rais Magufuli Akitoa siku 14 kwa Wamiliki wa Vituo vya Mafuta Nchini kutumia (EFDs).

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa baada ya kuzindua barabara hiyo.

Rais Magufuli leo July 19, 2017 ameanza ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Kagera ambako mbali na kuongea na Wananchi, amezindua barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa kilomita 154. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga imegharimu Tsh. Bilioni 190.4.
Rais Dkt. John Magufuli yupo kwenye ziara katika mikoa ya Kagera, Kigoma,Tabora na Singida ambako atafungua na kuzindua miradi 9 na Akizindua ujenzi wa barabara hiyo, Rais John Magufuli amesema kwamba Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umaskini na wananchi wanafanya ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.
Rais akiwapungia mkono wananchi wa Biharamulo.

Katika hatua Nyingine, Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kote nchini kutumia mashine stahiki za risiti za kielektroniki (EFDs) huku akisisitiza kuwa watakaoshindwa watafutiwa leseni zao.

Hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Prof. Philip  Mpango alivifungia baadhi ya vituo vya mafuta hapa nchini baada ya kubainika kuwa vilikuwa havitumii mashine stahiki za EFDs.

Rais akisalimiana na Wazee wa Biharamulo.

Kwa upande wake Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa amesema wanaunga mkono msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuendelea na masomo na wameanzisha shule ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad