Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Eng. Hamad Masauni (kushoto) akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari
Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam – Arusha, wakati alipofanya ziara
ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, Pwani.
Masauni mara
baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo
alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara
yake Bagamoyo.
Akiwa mjini
Chalinze, Masauni alizungumza na waendesha bodaboda na kuwapa maelekezo
kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani kwa kutobeba mishikaki,
uvaaji wa kofia ngumu na pia kufuata sharia zote za usalama barabarani.
|
Masauni (kulia) akizungumza na
waendesha bodaboda wa Mji wa Chalinze, wakati wa ziara yake.
“Mmenihakikishia
kwa wale ambao hamkua na kofia ngumu kuwa mkitoka hapa mtakwenda kuzitafuta,
hakikisheni mnafanya hivyo kwa usalama wenu pamoja na abiria mnaowabeba,
ipendeni kazi yenu kwa kuheshimu sharia za usalama barabarani,” alisema
Masauni.
Akiwa njiani
kuelekea Chalinze mpaka Bagamoyo, Masauni ambaye gari yake ilitolewa namba
zinazomtambulisha nafasi yake (NWMNN), na kuweka namba za kawaida ili kujua
kama akiendesha kwa mwendokasi barabarani matrafiki watalisimamisha gari lake,
hata hivyo askari wa usalama barabarani sehemu kubwa hawakuwepo barabarani na
pia waliokuwepo hawakuweza lisimamisha gari lake.
|
Masauni
(aliyevaa suti) akiwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha
Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani ambapo alifanya ziara ya kushtukiza kituoni
hapo.
Kutokana na
hatua hiyo, Masauni akagundua kuwa kuna uzembe mkubwa unaofanywa na matrafiki
mkoani humo kwa kutofanyakazi zao kwa umakini, na kwa uzembe huo ndio chanzo
cha ajali zinazotokea barabarani mara kwa mara.
Akizungumza
na Matrafiki wilayani Bagamoyo, ambao walifanya uzembe huo, aliwataka wabadilike
haraka iwezekanavyo kufuata wajibu wao, na pia alitoa siku tatu kuhakikisha
wanawakamata waendesha bodaboda wote ambao wanavunja sheria za usalama
barabarani, na pia baada ya operesheni hiyo apewe ripoti haraka iwezekanavyo,
na muda wowote atafanya ziara ya kushtukiza kuona kama maelekezo hayo
wameyafanyia kazi.
|
Masauni akimpa maelekezo Kamanda wa
Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus
Musilimu (kulia) wakati alipokua anazungumza na askari wa usalama barabarani
katika eneo la Sanzale, Bagamoyo.
“Bodaboda
nimeziona nyingi zinapita hapa zikiwa zinavunja sheria, madereva na abiria
hawajavaa kofia ngumu, na nyie mpo hapa mnaziangalia, sasa nawaagiza mtekeleze
maagizo niliyotoa na pia sio nyie tu bali nchi nzima wahakikishe wanayakagua
magari pamoja na bodaboda, na atakaepuuza atutacheka nae, tutapambana nae,”
alisema Masauni.
Kwa upande
wake Kamanda Msilimu, alisema ameyapokea maagizo yote na atahakikisha
anayafanyia kazi ipasavyo kwa kuwasimamia matrafiki wote nchini kwa umakini
mkubwa.
|
No comments:
Post a Comment