Tafakari Ajali Kahama-‘’Hii ajali nimejifunza Tanzania asilimia kubwa tunakufa kwa Uzembe’’. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 04, 2017

Tafakari Ajali Kahama-‘’Hii ajali nimejifunza Tanzania asilimia kubwa tunakufa kwa Uzembe’’.

Gari la Abiria namba T 702 CFT likiwa limeharibika baada ya kupata Ajali June 02,2017 majira ya saa tatu asubuhi ikitoka Kakola wilaya ya Msalala, Shinyang’a ikielekea Kahama ,Shinyanga kugongana na gari aina ya Toyota Land Cruiser namba T 221 DAP  na iliripotiwa kusababisha vifo 3 na majeruhi waliokimbizwa hospitali ya wilaya Kahama.

 Ajali hii imetokea eneo la  Ntobo karibu na kijiji cha Segese.

Anaandika Jackson Fundi- kuwa...''

-Moja uzembe wa madereva wetu speed naweza sema za kipumbavu.

-Pili Hakuna system za uokoaji au ni uzembe mkubwa kwa wahusika, Msaada kwenye hili tukio imechukua masaa mawili mpaka polisi kuleta gari la kubeba majeruhi na kilometa Kama 20 kufika Kahama mjini, taarifa ilitumwa in time. 

Majeruhi walikuwa wanachukuliwa na magari ya wasamaria wema. Watu wamepoteza maisha labda wangewaishwa hospital tungeokoa maisha yao.
Kitanda cha Kubebea Mgonjwa.

-Mbaya zaidi, hospital ndio shida kubwa Sana, mgonjwa kutolewa tu kwenye magari inachukua dakika zaidi ya 30.

- Mbaya zaidi hakuna hata first aid iliyotolewa na wauguzi zaidi ya kushangaa. 

-Mbaya kuliko yote angalia kitanda cha magurudumu kilicholetwa, Cha ovyo kina kutu, tuache hiyo kitanda kina damu ya mtu mwingine tunaweka mgonjwa mwingine mwenye kubleed, hata basi kutandikwa shuka.

TUTAMLUMU SANA RAIS JOHN POMBE MAGFULI KUTUMBUA WATU KWA UJINGA HUU.


Gari aina ya Toyota Land Cruiser namba T221 DAP  likiwa limeharibika vibaya kwa mbele baada ya ajali eneo la  Ntobo karibu na kijiji cha Segese.

Post Bottom Ad