SportPesa-Yanga SC usoni mwa AFC Leopards,Simba SC kujiuliza Leo June 6,2017 kwa Nakuru All Stars. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 06, 2017

SportPesa-Yanga SC usoni mwa AFC Leopards,Simba SC kujiuliza Leo June 6,2017 kwa Nakuru All Stars.

Ubingwa wa kuwania Kombe SportPesa SUPER CUP 2017, inayodhaminiwa na SportPesa Kampuni ya Kuchezesha Michezo ya Bahati Nasibu Mitandaoni, imeaanza Jana June 5,2017 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC na AFC Leopards ya Kenya watakutana uso kwa uso katika Nusu Fainali baada ya kufuzu kwa changamoto ya Matuta baada ya Sare ndani ya Dakika 90.

Kwenye Mechi ya Kwanza, Timu Mpya ya Ligi Kuu Vodacom, Singida United, inayoongozwa na Kocha wa zamani wa Yanga SC, Hans van der Pluijm, ilitangulia kufunga Bao Dakika ya 20 kupitia Pro wao kutoka Zimbabwe Kutinyu Tafadzwa.

Lakini AFC Leopards walisawazisha Dakika ya 63 kupitia Vincent Oburu.

Hadi Dakika 90 kwisha Gemu ilibaki 1-1 na ikaja Tombola ya Mikwaju Mitano ya Penati ambapo AFC Leopards walifuzu kwa Penati 5-4.

Baada ya Mechi hii wakaingia Yanga SC ambao walitoka 0-0 na Tusker FC ya Kenya lakini kufuzu kwa Penati 4-2 .
Tusker FC walifunga Penati 2 wakati moja ikiokolewa na Kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na nyingine kutoka nje baada kuparaza Posti.

RATIBA.

Jumanne Juni 6,2017

Saa 8 Mchana Simba v Nakuru All Stars

Saa 10 na Robo Jioni Gor Mahia v Jang’ombe Boys

Alhamisi Juni 8,2017.

Nusu Fainali

Saa 8 Mchana AFC Leopards v Yanga

Saa 10 na Robo Jioni Mshindi RF3 v Mshibdi RF 4

Jumapili Juni 11,2017.

Fainali

Saa 10 Jioni

Post Bottom Ad