Picha 12 za Huzuni na Furaha wakati Real Madrid wanachukua Ubingwa wa 12 wa Champions League 2016/2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 04, 2017

Picha 12 za Huzuni na Furaha wakati Real Madrid wanachukua Ubingwa wa 12 wa Champions League 2016/2017.

Mabingwa Ulaya Real Madrid na furaha ya Ushindi.

Klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania imeichakaza Juventus ya Italia 4-1 na kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Fainali ya UEFA Champions League 2016/2017 iliyochezwa huko Millenium Stadium, Jijini Cardiff, Wales Jana June 3, 2017 huku ikiweka rekodi ya kuwa  klabu ya kwanza kuchukua Ubingwa mara mbili mfululizo.

Hii ni mara ya 12 kwa Real Madrid kuwa Mabingwa wa Ulaya.

Kwa Juventus,ya Italia ambao wameshinda Fainali zao mbili tu kati ya Nane walizotinga, sasa wamefungwa katika zote Tano walizofika mara ya mwisho ambazo ni za Miaka ya 1997, 1998, 2003, 2015 na hii ya 2017.

Tangu AC Milan wafanikiwe kutetea Ubingwa wa Ulaya Miaka ya 1989 na 1990, wakati huo Kombe hili likiitwa, EUROPAEN CUP, hakuna Timu iliyowahi kutetea Taji hili la UEFA Champions League hadi hii fainali ya Jana June 3, 2017 na Real Madrid kuweka Historia hii.
Kwa Mchezaji Bora Duniani sasa amefikisha Maba 105 ya Champions League na Msimu huu wa 2016/2017 ni Cristiano Ronaldo ndie Mfungaji Bora wa Mashindano haya akiwa na Bao 12 akimpiku Lionel Messi wa FC Barcelona aliefunga Bao 11.


Mchezaji Cristiano Ronaldo ameshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mara Nne sasa - mara tatu akiwa na Real Madrid na Moja akiwa na Manchester United.

Mreno Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili, la kwanza kwake na klabu dakika ya 20 na lake la pili dakika ya 64 kutoka kwa krosi ya Luka Modric.

Casemiro aliwafungia Real bao lao la pili dakika ya 61 kabla ya Marco Asensio kukamilisha ushindi wao dakika ya 90 kwa bao lao la nne.

Juventus, waliokuwa wameanza vyema mechi hiyo wakikuwa wamekomboa bao la kwanza la Ronaldo dakika ya 27 kupitia Mario Mandzukic na kufanya mambo kuwa sare wakati wa mapumziko lakini kipindi cha pili mawimbi yaliwageuka.


Real Madrid wamefanikiwa kuwa klabu ya kwanza tangu AC Milan (1989, 1990) kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya misimu miwili mfululizo, na ni mara yao ya 12 kushinda kombe hilo.

Mwaka huu ni mara ya tatu kwa Real Madrid kufika fainali katika misimu minne.

Kipa Gianluigi Buffon.

Juventus ndiyo klabu pekee ambayo ilikuwa haijashindwa mechi yoyote msimu huu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, klabu ya kwanza tangu Atletico Madrid mwaka 2013/2014 kufika fainali bila kushindwa.

Kushindwa kwa Juventus ni pigo kubwa kwa nahodha wao, mlinda lango Gianluigi Buffon, 39, ambaye hajawahi kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kabla ya mechi, alikuwa amesema ushindi ungekuwa na maana kubwa sana kwake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad