Makamu Wa Rais-Viwanda na Migodi Vinavyoharibu Mazingira Vichukuliwe Hatua Kali. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Monday, June 05, 2017

Makamu Wa Rais-Viwanda na Migodi Vinavyoharibu Mazingira Vichukuliwe Hatua Kali.

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi (hawapo pichani) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Jana June 04,2017 Mjini Butiama mkoani Mara.Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu akiongea na mjane wa Rais wa Kwanza wa Tanzania Baba wa Taifa Julius Kambarage, Mama Maria Nyerere (kulia).

Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa viwanda na migodi inayofanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwamo utitirishaji wa kemikali  katika makazi ya watu.

Amesema  kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine.

Mama Suluhu Hassan ametoa agizo hilo Juni 4,2017 kijijini Butiama mkoani Mara wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.

Amesema uharibifu wa mazingira ukiachwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe na hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo.

Kutozingatia hifadhi ya mazingira kunaweza kusababisha kuparaganyika kwa mfumo wa ikolojia  na kufanya maisha yetu na ya vizazi vijavyo kuwa mashakani,” amesema

Aliongeza kuwa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

Post Bottom Ad