Kocha Zinedine Zidane na Cristiano Ronaldo Waweka Rekodi hii Ligi ya Mabingwa Ulaya. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Sunday, June 04, 2017

Kocha Zinedine Zidane na Cristiano Ronaldo Waweka Rekodi hii Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Orodha ya Wafungaji Klabu Bingwa Ulaya 2016/2017.

Mchezaji Cristiano Ronaldo ameithibitishia dunia yeye ni mchezaji wa aina yake baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitano mfululizo.

Ronaldo amefunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiitwanga Juventus kwa mabao 4-1 na kube Ubingwa wa Ulaya wa Msimu huu wa 2016/2017.

Mabao hayo mawili yamemfanya amfikie na kumvuka mpinzani wake, Lionel Messi wa Barcelona ambaye alikuwa na mabao 11.

MISIMU.

2017- Mabao 12

2016- Mabao 16

2015-Mabao 10

2014- Mabao 17

2013-Mabao 13.
Nae Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kulitetea Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Zidane ameiongoza timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo.


Hivyo, rekodi ya kocha aliyebeba kombe hilo mara mbili au kulitetea inakwenda kwa raia huyo wa Ufaransa ambaye amewahi kuzichezea kwa mafanikio Juventus na baadaye Madrid.

Post Bottom Ad