Kaburi la Ivan Ssemwanga Kufukuliwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 02, 2017

Kaburi la Ivan Ssemwanga Kufukuliwa.

Vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa mwanasheria mmoja ameiomba mahakama itoe ruhusa ya kufukuliwa kwa kaburi la aliyekuwa mfanyabaishara maarufu kutoka Uganda akiishi Afrika Kusini, Ivan Semwanga.

Bilionea huyo ambaye pia alikuwa mume wa Zari The Boss Lady alizikwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichomwagwa kwenye kaburi lake na waliokuwa rafiki zake wanaofahamika kama ‘Rich Gang.’
Mwanasheria, Tugume Gideon ameiomba Mahakama Kuu ya Uganda kutoa kibali hicho ili fedha hizo ziweze kutolewa kaburini, kwani ni kinyume na sheria kufukia fedha ardhini ambazo ni moja ya nyara za serikali.

Ivan Semwanga alizikwa siku ya Jumanne May,30,2017 nyumbani kwake Kayunga nchini Uganda.


Post Bottom Ad