Yussuf Manji Ajiuzulu Wadhifa wa Uenyekiti Yanga SC. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, May 23, 2017

Yussuf Manji Ajiuzulu Wadhifa wa Uenyekiti Yanga SC.

Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amejiuzulu wadhifa  huo akidai kuwa anatoa nafasi kwa watu wengine kuiongoza.

Barua iliyosainiwa na Yusuf Manji Mei 22, 2017 inaonesha kwamba Manji ameachia rasmi nasasi ya uenyekiti wa klabu ya Yanga SC na makamu Mwenyetiki wa klabu hiyo Clement Sanga atakuwa Mwenyekiti na kuiongoza klabu hadi hapo uchaguzi utakapofanyika ili kumpata Mwenyekiti mpya.

Kwa mujibu wa maelezo ya barua, Manji alifikia uamuzi wa kujiuzulu Mei 20 mwaka huu siku ambayo Yanga SC ilitangazwa kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2016/2017.

Katika barua hiyo, Manji amsema ameamua kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa wengine nao kushika uongozi ndani ya klabu hiyo.

HAPA CHINI ISOME BARUA YOTE.


Post Bottom Ad