Yanga SC-Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2016/2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 20, 2017

Yanga SC-Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2016/2017.


Kikosi cha Yanga SC kimefanikiwa kutetea ubingwa wake wa VPL msimu huu 2016/2017  ikiwa ni mara ya tatu mfululizo tangu walipolitwaa taji hilo msimu wa 2014/2015 hadi sasa 2016/2017.

Licha ya kufungwa ugenini na Mbao FC kwa goli 1-0, bado kipigo hicho hakikuizuia Yanga SC kushinda taji hilo kutokana na wastani mzuri wa magoli waliokuwa nao dhidi ya mpinzani wao Simba SC.

Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara lililofungwa leo May 20, 2017 ni kwa vigogo, Simba SC na Yanga SC kumaliza wakiwa sawa kwa Pointi 68 kila moja baada ya mechi 30.

Hiyo inafuatia Simba SC kuibuka na ushinid wa 2-1 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Yanga SC wakichapwa 1-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa matokeo hayo, Yanga SC inafanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu kwa wastani wake mzuri wa mabao, ingawa bado kuna tishio la Simba SC kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) mjini Zurich, Uswisi kudai pointi tatu za chee walizopokonywa baada ya kupewa kimakosa kufuatia kufungwa na Kagera Sugar.

Rasmi sasa timu tatu zilizoteremka daraja kutoka Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara msimu huu 2016/2017 zimejulikana nazo ni JKT Ruvu kutoka Pwani, Toto African ya Mwanza na African Lyon ya Dar es Salaam.

Toto African wamepoteza kwa kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar wakiwa ugenini mjini Manungu, Morogoro na Ndanda FC wakawashindilia zaidi JKT kwa mabao 2-0 ambao tayari walikuwa wameishateremka.

Kwa African Lyon, wao walionekana kama walikuwa wanaweza kubaki lakini sare yao ya 0-0 ikishindwa kuwaokoa katika mehi ya mwisho.

Matokeo ya mechi nyingine Kagera Sugar imeifunga Azam FC bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Stand United imeilaza 2-1 Ruvu Shooting Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Majimaji  FC imeshinda magoli 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja Maji Maji Songea.


Hiyo inamaanisha, JKT Ruvu, Toto Africans na African Lyon ndizo zinaipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu, zikizipisha Mji Njombe, Lipuli ya Iringa na Singida United zilizopanda kutoka Daraja la Kwanza.

Post Bottom Ad