Ufafanuzi wa Polisi Kuhusu Ndege kutua Barabarani -Dodoma. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Friday, May 12, 2017

Ufafanuzi wa Polisi Kuhusu Ndege kutua Barabarani -Dodoma.

Picha za ndege hiyo.

Baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao kuwa kuna ndege imetua barabarani mkoani Dodoma, Polisi mkoani humo wamesema hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa hizo.
Picha za ndege hiyo.

 
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amesema  taarifa sahihi ni kwamba hiyo ndege ni scrapper, ilikuwa ni ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, ilikuwa airport na ilishafutwa kwenye ndege za jeshi na ni kopo tu wala haina engine  nzima.

“Muhusika ambaye aliinunua kwenye mnada jana alikuwa anaikokota kwa kuivuta na tractor kupitia hiyo hiyo barabara ya airport.  Sasa wakati anaivuta katika kupishana na magari, tairi zikateleza na kuingia kwenye zile kingo za barabara, baada ya hapo wakaitoa na kuendelea na safari yao. Jana nikapigiwa kuwa kuna ajali lakini ukweli ni kwamba hakukua na ajali,” Mambosasa ameimbia Clouds Fm.

Post Bottom Ad