Taswira Picha za Msiba wa Taifa, Mkoani Arusha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 09, 2017

Taswira Picha za Msiba wa Taifa, Mkoani Arusha.

Majeneza yenye miili ya marehemu yakishushwa kwenye gari na kupelekwa sehemu maalum kwa ajili ya kuagwa.

Ajali hiyo iliyotokea Jumamosi,May 06,2017 iliyopita katika Kijiji cha Marera kwenye Mlima wa Rhotia wilayani Karatu wakati wanafunzi hao wakielekea kwenye ziara ya kimasomo kwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema na Shule ya Tumaini Academy iliyopo mjini Karatu.

Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba basi hilo walilopata nalo ajali aina Toyota Coaster lenye namba za usajili T 871 BYS lilikuwa kati ya mabasi matatu ya shule hiyo yaliyokuwa yameongozana na taarifa kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa basi hilo lilikuwa katikati ya mengine.

NINI CHANZO CHA AJALI?

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wakati basi hilo linapita mji mdogo wa Rhotia Hill lilikuwa katika mwendo mkali bila kujali wingu zito lililokuwa limetanda na mvua iliyokuwa ikinyesha huku barabara ikiwa na utelezi kutokana na aina ya udongo wa eneo hilo ambao ulikuwa umeingia barabara pamoja na kwamba ni barabara ya lami.

Inaaminika kuwa, udongo huo ndiyo ulifanya tairi kuteleza hivyo kukatika kwa breki kwenye mteremko huo mkali ambao pia kuna daraja.

Walidai kuwa, basi hilo lilikuwa linashuka kwa kasi kwenye mteremko mkali wa Mlima Rhotia katika makutano ya Barabara ya Kwa-Karani huku wanafunzi hao wakipiga kelele za kuomba msaada.

Mashuhuda hao walisema walishangaa kuona basi hilo likipaa na kutumbukia katika korongo refu la Mto Marera unaopatikana wilayani Karatu na kusikika kishindo kikubwa ndipo watu wa eneo hilo wakakimbilia na kuanza kutoa msaada.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa Jana May 08,2017.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili hiyo.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na chama wakiwa kwenye uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent.


Wanafunzi wa shule ya Lucky Visent wakiwa kwenye majonzi wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa  katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent waliofariki kwenye ajali.

Post Bottom Ad