Taswira Namna Rais Dkt.Magufuli alipomuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 29, 2017

Taswira Namna Rais Dkt.Magufuli alipomuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.

Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo Leo May 29,2017 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli alimteua tarehe 28 Mei, 2017 Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Polisi (IGP).

Kabla ya Uteuzi huo IGP Simon Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

IGP Simon Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Picha namba Juu na Chini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha vyeo vipya Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro kabla ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.


 
Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akisaini Hati ya Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba,IGP mpya Simon Sirro,  IGP wa zamani Ernest Mangu pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Magereza.
 

  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro pamoja na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Majeshi ya Polisi na Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba mara baada ya tukio la uapisho wa IGP Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Post Bottom Ad