Taswira -Majeruhi watatu wa ajali ya Basi la Wanafunzi la Lucky Vicent walivyosafirishwa kwenda Marekani kwa Matibabu zaidi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 14, 2017

Taswira -Majeruhi watatu wa ajali ya Basi la Wanafunzi la Lucky Vicent walivyosafirishwa kwenda Marekani kwa Matibabu zaidi.

Majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi la Lucky Vicent wakipakiwa kwenye Ndege ya Taasisi ya Samaritan's Purse ambao wamejitolea kuwahudumia kwa matibabu majeruhi hao kwa kuwasafirisha nchini Marekani kwa Matibabu zaidi huku majeruhi hao wakiongozana na wazazi wao, daktari mmoja na nesi mmoja kwa kila majeruhi.

 Picha kwa Msaada wa Mtandao wa Whatsapp.

Baadhi ya wananchi, ndugu jamaa na wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha waliojitokeza kwa ajili ya kuwasidikiza majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky Vicent iliyotokea wiki iliyopita huko Karatu Arusha Tanzania.

Majeruhi watatu wa ajali ya basi la wanafunzi la lucky Vicent iliyotokea wiki iliyopita wilayani Karatu Mkoani Arusha na kupoteza watu takribani 34 leo wamesafirishwa na Ndege ya taasisi ya Samaritan's Purse kuelekea nchini Marekani kwaajili ya kupatiwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata kutokana na ajali hiyo iliyopelekea kupoteza maisha ya wenzao 30, dereva 1 na walimu wawili.

Majeruhi hao ambao ni Doreen Mshana (13), Sadia Ismael Awadhi (11) na Wilson Geofrey Tarimo (11) wameongoza na wazazi wao huku kila mmoja akiwa na usaidizi wa daktari mmoja na nesi mmoja kutoka hospitali ya Mount Meru Arusha.

Mwanawamakonda Blog inapenda kuwatakia safari njema ya matibabu yao Na Mungu akapate kuwaponya haraka ili kusudi wareje kuendelea na maandili ya mtihani wao wa taifa wa Darasa la Saba.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Bw Mrisho Gambo akiwa pamoja na wazazi wa majeruhi wa ajali ya wanafunzi wa Lucky vicent katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA kabla ya safari ya kuelekea Marekani kwaajili ya matibabu yaliyotolewa na taasisi ya Samaritan's Purse, Ajali hiyo iliyotokea wiki iliyopita huko Karatu mkoani Arusha na kupoteza maisha ya Wanafunzi, walimu na dereva kufikia 35.

Ndege ya Taasisi ya Samaritan's Purse ikiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mapema leo asubuhi tayari kwa kuruka mpaka Marekani kwaajili ya kuwapeleka majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky vicent iliyotokea May 6,2017 na kupoteza watu 35 huko Karatu mkoani Arusha,Tanzania.

Sehemu ya ndani ya Ndege ya Samaritan's Purse iliyowabeba majeruhi watatu wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ambao leo wamesafirishwa kuelekea nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi huku gharama za matibabu hayo yakitolewa na taasisi ya Sammaritan's Purse.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad