Tanzia: Mzee Philemon Ndesamburo Afariki Dunia. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 31, 2017

Tanzia: Mzee Philemon Ndesamburo Afariki Dunia.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro na (Chadema), Mzee Philemon Ndesamburo ameafariki dunia muda mfupi uliopita baada ya kuanguka ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya KCMC.

Taarifa za awali zimeelea kuwa, Mzee Ndesamburo alikuwa ofisini kwake akimwandikia cheki ya benki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro kwa ajili ya kutoa rambirambi ya vifo vya watu 35 wakiwemo wanafunzi, walimu na dereva wa Shule ya Msingi, Lucky Vincent, Karatu ambapo kabla hajamalizia kuandika, hali yake ilibadilika ghafla. 

Meya aliamchukua na kumkimbiza hospitali ambapo kabla hajaanza kutibiwa alipoteza maisha.

Katibu wa Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mhe. Amani Golugwa amethibitisha.

Post Bottom Ad