TANROAD KAGERA-Hii mmekiacha pale kama maonesho? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, May 05, 2017

TANROAD KAGERA-Hii mmekiacha pale kama maonesho?

Naomba nianze na hili maana ndilo ninaloona lina maslahi mapana kwa ustawi wa usalama wetu barabarani.

Mwishoni mwa mwezi wa tatu kama sio mwanzoni mwa April, mwaka huu 2017 eneo la Kasharazi kwa Nkhuru  hapa wilayani Ngara,mkoani Kagera kulitokea ajali nne within a week zote zikihusisha magari makubwa na ajali ya lori la mwisho lilikuwa limebeba Makaa ya Mawe nadhani yalikuwa yanaelekea Burundi.

Cha ajabu ni mwezi kama sio zaidi ya mwezi hapa ,hili gari lilipopatia ajali na yale makaa kumwagika barabarani hakujasafishwa kuondoa kile kifusi sasa najiuliza mmekiacha pale ili kutokee ajali nyingine au mmekiacha pale kama maonesho?
Maana kwanza ni kwenye kona,pili ni kwenye miteremko anayetokea K9 hawezi kumwona anayetokea huku Ngara mjini na anayetokea Mjini obvious hawezi mwona anayetokea K9. 

Nadhani TANROAD hamko serious na ninyi mnaojiita mabalozi wa usalama barabarani hili mnashindwa kulisemea kweli? 

Ni majuzi tu nimeshuhudia gari zinakosana kugongana na zote zilikuwa speed. Na bet kabisa kama hamtatoa hiki kifusi cha haya makaa basi mtegemee ajali mbaya zaidi itakayokuja kusababishwa na hiki kifusi.
Na-Sinzo Jr Sinzo

Post Bottom Ad