Swaga za Chelsea kuelekea Ubingwa Ijumaa May 12,2017 wakishinda dhidi ya West Brom. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 09, 2017

Swaga za Chelsea kuelekea Ubingwa Ijumaa May 12,2017 wakishinda dhidi ya West Brom.

Timu ya Chelsea imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu England 2016/2017 baada ya kuitwanga Middlesbrough Bao 3-0 na kuishusha Daraja huku wao wakisubili ushindi kwenye Mechi moja tu ili watwae Ubingwa huo wa Ligi.

Sasa Chelsea wanaweza kuwa Mabingwa Ijumaa May 12,2017 wakiwa na mechi 2 mkononi ikiwa watashinda Ugenini huko The Hawthorns watakapocheza na West Bromwich Albion.

Matokeo haya ya nyumbani Stamford Bridge, Jijini London Leo yamewaunganisha Middlesbrough, maarufu kama Boro pamoja na Sunderland kuteremshwa Daraja na sasa watacheza Daraja la chini ya EPL, la Championship, Msimu ujao.

Chelsea walifunga Bao lao la Kwanza Dakika ya 23 kwa Pasi safi ya Cesc Fabregas na Diego Costa kukwamisha Mpira Wavuni.

Bao la Pili la Chelsea liliingia Dakika ya 34 Mfungaji akiwa Marcos Alonso aliemalizia Krosi ya Azpilicueta.

Dakika ya 65 alikuwa tena Cesc Fabregas aliemsukia Nemanja Matic kupiga Bao la 3 na Chelsea kuongoza 3-0 Bao zilizodumu hadio mwisho.

LIGI KUU ENGLAND-2016/2017.

Ratiba

Jumatano Mei 10,2017.

2145 Southampton v Arsenal               

Ijumaa Mei 12,2017.

2145 Everton v Watford             

2200 West Bromwich Albion v Chelsea            

Jumamosi Mei 13,2017.

1430 Manchester City v Leicester City            

1700 Bournemouth v Burnley               

1700 Middlesbrough v Southampton    

1700 Sunderland v Swansea City

1930 Stoke City v Arsenal

Jumapili Mei 14,2017.

1400 Crystal Palace v Hull City   

1615 West Ham United v Liverpool      

1830 Tottenham Hotspur v Manchester United 

Post Bottom Ad