Rekodi ya Manchester United baada ya Ubingwa akiungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City -Klabu Bingwa Ulaya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 25, 2017

Rekodi ya Manchester United baada ya Ubingwa akiungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City -Klabu Bingwa Ulaya.

Picha ya Furaha ya Ubingwa 2016/2017.

Manchester United wameshinda fainali ya Kombe la Europa kwa kuifunga Ajax Amsterdam kwa mabao 2-0 mjini Stockholm Sweden.

Magoli ya Mchezaji Paul Pogba na Hendrick Mkhitaryan yameipa Man United sio tu Kombe bali pia nafasi ya kucheza Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao wa 2017/2018.

Manchester United sasa wanaungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City katika kucheza Klabu Bingwa Ulaya. 

Pia ushindi huu utawaingizia kitita cha takriban Pauni milioni 50.


Hili ni kombe la Pili kwa Kocha Mourinho anashinda na Man United katika msimu wake wa kwanza. Man United walishinda Kombe la Ligi mwezi Februari.

Pia -Jose Mourinho ameshinda Fainali zote 4 za Ulaya alizotinga kama Meneja akitwaa UEFA CUP 2003 na UEFA Champions League 2004 akiwa na FC Porto, na UEFA Champions League 2010 akiwa na Inter Milan.

Mourinho amedumisha rekodi yake ya 100% ya ushindi dhidi ya Ajax katika Mechi zote 7 alizocheza nao.

Man United wamejumuika na Ajax, Bayern Munich, Chelsea na Juventus kuwa Klabu pekee zilizonyakua Makombe yote ya UEFA huko Ulaya.

-Vikombe hivyo ni UEFA Champions League, UEFA Cup Winners' Cup, UEFA Cup/UEFA EUROPA League.

Jose Mourinho Ameeleza: “Ni mwisho wa Msimu mgumu. Lakini ni Msimu mzuri mno!”

Aliongeza: “Tulipendelea kufuzu UEFA Champions League kwa njia hii kupita ile ya kumaliza Nafasi ya 4, 3 au 2! Tumetimiza lengo kwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Ulaya, Taji muhimu. Sasa Klabu ina kila Taji Duniani!
 






Kocha Jose Mourinho.

Mourinho alieleza: “Sasa tuna heshima ya kucheza UEFA SUPER CUP na Bingwa Mpya wa UEFA Champions League kati ya Real Madrid au Juventus watakaocheza fainali ya Champions League June 03,2017, kwa hiyo Msimu huu ulikuwa mzuri mno!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad