Rais Yoweri Museveni -Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 20, 2017

Rais Yoweri Museveni -Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es salaam kabla ya kuana Mkutano wa 18 wa wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mei 20,2017.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es salaam kabla ya kuana Mkutano wa 18 wa wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mei 20,2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na kumkaribisha Mhe. Gaston Sindimwo Makamu wa Rais wa Burundi Ikulu jijini Dar es salaam kabla ya kuanza Mkutano wa 18 wa wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mei 20,2017.

Rais John Magufuli leo May 20, 2017 (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.

Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani.

“Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana 2016.

Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.
Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.

Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo wake wote.

Post Bottom Ad